Wednesday, December 28, 2005

KASI MPYA YAZIDI KUPINDUA VIGOGO CCM-SASA NI ZAMU YA BABU MSEKWA, AANGUKIA PUA.

Ni punde tu nimetoka kuangalia kinyang’anyiro cha uspika wa bunge letu tukufu na ningependa kuwashirikisha matokeo hayo na changamoto aliyoitoa Spika mpya aliyechaguliwa Mheshimiwa Samwell Sitta.

Hakuna shaka kua ushindi wake ulitabiriwa na wengi ila tofauti ya kura alizompita mpinzani wake wa karibu bwana Msekwa ni kielelezo kingine kilicho wazi kua tayari ndugu msekwa na naibu wake walikua hawana mvuto wowote katika bunge lililopita na kitu kilichokua kinasubiriwa ni muda ufike na hatimaye kuwaaga rasmi tena kwa aibu iliyo kuu.Spika mteule amepata kura 217 huku bwana Msekwa akiambulia kura 57 na aliyekua naibu wake amefanikiwa kupata kura yake pekee, yaani kura moja.

Mheshimiwa spika mteule anayejiita “THE MAN OF STANDARDS AND SPEED” ameanza kwa kutoa onyo kali kwa mawaziri watakaoteuliwa kua wajiandae na mijadala mikali itakayozingatia na kuweka mbele maslahi ya taifa kwani wakati wa mzaha umekwisha na kilichobaki ni kusogeza gurudumu la maendeleo kwa Ari mpya,kasi mpya na nguvu mpya “Majibu yasiyojitosheleza hayatavumiliwa na bunge hili” nimemnukuu mheshimiwa spika akiwasihi Mawaziri wateule wajiandae.Yetu macho kwani tumewazoea kwa maneno matamu na utendaji sifuri.

Nafikiri wanablog mnaweza mkazua maswali mengi katika hili,Je bunge lililopita lilikua ni la mzaha siyo? Je msekwa alikua hatoi nafasi kwa ajili ya mijadala hiyo?Je bunge lilikua limepoteza imani kwa Msekwa na Akukweti kwa kiasi hicho?Je falsafa ya ari mpya inataka sura ngeni?Lakini mbona Sitta si mgeni katika System?

Labda nimalizie kwa kutoa wito kwa mheshimiwa msekwa kwasasa ajikite zaidi katika masomo yake ya shahada ya kwanza ya sheria katika chuo kikuu huria cha Tanzania angalau aweze kusajiliwa kama wakili wa kujitegemea ili awasaidie raia kama nia yake kweli ni utumishi!

3 comments:

boniphace said...

Asante Materu nilichelewa kupitia hapam kwako lakini nilipata taarifa kama hizi kutoka Dar usiku na kuzipachika kwangu ila sikuwa na matokeo. Nafurahi na sisi tunapigia mstari hapo kwenye mzaha, na mijadala na kisha suala la mahudhurio la vikao vya Bunge.

Kila la heri hii ni bakora ya kwanza aliitaka Msekwa kaipata na safari inaendelea nami naungana nawe aende shule akamalize shahada hiyo kisha anaweza kupata Uanasheria Mkuu katika serikali ijayo.

FOSEWERD Initiatives said...

Aksante sana bwana materu kwa changamoto hii. kwanza japo si lazima sana elimu kuwa sambamba na uwezo wa kufanya kazi, lakini elimu ni nyenzo muhimu katika kufanya maamuzi ikiwa tu haikufunikwa na ubinafsi. kwa kweli nimepigwa na bumbuazi kuona kuwa katika nchi iliyojaa wasomi tulikuwa na spika ambaye hakuwahi kuandika walau thesis!! hata hivyo sishangai sana kwa hilo kwani kuna mambo mengi yalikuwa yanaendelea bungeni na huyu bwana alikuwa hawezi kuelekeza kuwa huu ni utani na hii ni hali halisi. ni kweli kuwa huyu bwana alikuwa anachekea majibu ya ovyo ovyo. wabunge wengi walionekana wabaya kwa sababu alikuwa hawasapoti kupata majibu ya matatizo yao. kama utakumbuka hakuna shilingi iliwahi kuondolewa kipindi hiki. ninaamini ukiwa umeenda shule unakuwa muumini wa taaluma na unafanya kazi kufuata taaluma zaidi. mh. sitta kama mwanasheria ninampa nafasi kuubwa sana ya kujiamini katika nafasi yake mpya. KITENDO CHA KUTAMBUA KUWA ANA MAMLAKA JUU YA MAWAZIRI NA HIVYO KUTOA MAAGIZO YAKE MWANZONI KABISA NI USHINDI MKUBWA - NADHANI MSEKWA KAMA ALIKUWA ANALIJUA HILO BASI ALIKUWA HAJIAMINI! hilo pia ni bomba. natumaini Tunamwomba pia mh. Sitta awe mlezi wa demokrasia kwa kuvipa vyama vya upinzani chumba cha kupumulia kwa mustakabali wa taifa. asipende sana kugeuza bunge kuwa kamati ya chama.

unajua kumbe huyu angegusa daftari la mlimani kidogo angemshauri hata mkewe - mama anna kuwa makini na kuelewa matatizo ya madaktari wetu wapendwa!! buh buh buh !

cheers