Wednesday, November 30, 2005

KAMATA KAMATA YA VIONGOZI WA UPINZANI NA MUSTAKABALI WA AMANI ZANZIBAR.
Zikiwa zimepita takribani siku thelathini(30) tangu kumalizika kwa uchaguzi visiwani zanzibar na hatimaye kupatikana mshindi ambayeni Mh. Aman Abeid Karume wa C.C.M ni wazi kua hakuna atakeyethubutu kusimama na kujidai mbele ya watu wenye fikra thabiti,makini na ang'avu kua hali ya kisiasa zanzibar ni shwari.

Kutapakaa kwa vikosi vya ulinzi na usalama mitaani ni ishara tosha kua hali ya mambo visiwani humu bado si shwari kama wenzetu washikao HATAMU wapendavyo tuamini.Kila kona utawaona askari wakiwa ndani ya sare zao wakitembea kwa miguu huku wamesheheni silaha za kila aina na wengine wakirandaranda ndani ya magari yao ambalo limekua jambo la kawaida kwasasa.INABIDI KATIKI HILI WANABLOG WENZANGU TUHOJI KWANINI?

Kwa upande mmoja chama kikuu cha upinzani(CUF) kinatafsiri hali hii kama njia ya kuwatisha viongozi na wafuasi wake ili wasijitokeze kwenye kampeni na baadaye kupiga kura za kumchagua Rais wa jamhuri ya Muungano,Wabunge na madiwani hapo Tar 14 december ili kukwepa fedheha ya kushindwa kwa chama tawala katika kinyang'nyiro hiki.Hali visiwani humu inazidi kua mbaya na kuzua wasiwasi mkubwa ukiambatana na maswali mengi baada ya kukamatwa kwa Mgombea Ubunge wa jimbo la Magogoni Mh. Abdulrahman Dedes amabye anafanya idadi ya viongozi wa cham hicho wakiokamatwa hadi sasa kufikia watatu baada ya mkurugenzi wa vijana na uchaguzi na mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama hicho.

Hali hii inapaswa kuwa changamoto kwa Rais Karume ambaye ameonyesha kua Muumini mzuri wa Muafaka ambao sasa unaonekana uko taabani baada ya chama kikuu cha CUF kukataa kutambua matokeo.

NAAMINI YA KUA SIASA HIZI ZA KUPANIANA NA KULIPIZANA VISASI HAZITAFIKISHA KISIWA HIKI POPOTE KATIKA HARAKATI ZAKE TEKETEKE ZA KUJIKWAMUA KATIKA GIZA HILI NENE LA UMASKINI!KWANINI MSIKAE,MJADILIANE,MKUBALIANE NA KUAMUA MAMBO CHANYA YA MAENDELEO NA SI KUNDELEZA CHUKI AMBAZO MWISHO WAKE TUNAUONA HAUNA ISHARA NJEMA!

Mheshimiwa KARUME na askari wako wa miavuli hebu jaribu kutumia busara katika hili.

4 comments:

boniphace said...

Materu sasa unakuwa mtu mzima. Hongera lakini bado andika tathmini ya ulivyoona uchaguzi oooh nimesahau kuwa ulikimbilia Dar kwa hofu ya polisi lakini waweza pia kuandika kisa cha wewe kukimbilia Dar kabla ya uchaguzi huo

Ndesanjo Macha said...

Gasper, ukiweza kupiga picha moja au mbili kiwiziwizi za hawa wana "usalama" ingekuwa poa sana. Unaweza?

FOSEWERD Initiatives said...

materu,

ninalifanyia kazi oni lako la kujadiliana ni kwanini watu wanapenda sana kutawala!

cheers

FOSEWERD Initiatives said...

jibu la kwanza hilooooo

nilikuahidi nitakupa majibu kwa nini watu wanapenda sana kutawala!

ninadhani sasa kuna haja ya kurejea tafsiri za neno kazi kama ilivyotasfsiriwa katika ibara ya ??? ya katiba ya ccm- kuwa ni shughuli yoyote ya halali inayomwingizia mtu kipato!! - nadhani inabidi pale mbele kuongeza ISIPOKUWA SIASA!

watu hawataki kujibidiisha kitaaluma na kujitahidi kujitegemea kimaisha na hivyo kuchukua njia mkato kusimama jukwaani na baadae kugombea uspika! - hawa hawana lingine la kutegemea kimaisha!

megine yanakuja

cheers