Thursday, December 15, 2005

ISHARA YA USHINDI WA CUF KATIKA JIMBO LA MJI MKONGWE.
Ni kama masaa mawili tu yamepita tangu alipotangazwa MAALIM SANYA kua ndo mshindi wa kiti cha ubunge katika jimbo la mji mkongwe.Wafuasi wa chama cha CUF wlilipuka kwa shangwe kuu huku wakichukua tahadhari kubwa wakati wa hekaheaka zao za kushangilia ushindi kwani vikosi vya usalama vimetapakaa kila kona za mji huo uliozoeleka kua na pilika nyingi wakati wa mchana.

Tunaweza kusema kua ni kama kiini macho kwa chama tawala tawala kwani watakua hawaamini nini kimetokea licha ya kutumia nguvu kubwa katika harakati zake za kukomboa jimbo hilo lililopo mikononi mwa wapinzani tangu mwaka 1995.Tangu jana asubuhi kumekuwepo na lawama za kupandikizwa mamluki wakiwa katika sare za kiusalama kwa ajili ya upigaji kura na hadi sasa hakuna ufafanuzi wa kina uliotolewa na Tume ya uchaguzi ya ZEC.

Nikiwa katika harakati zangu za kuelekea eneo maarufu la darajani kama kiunganishi cha mji huo mkongwe niliponea chipuchupu kutiwa ndani ya wana usalama waliokua wakiranda kila kona za njia ya mji huo wakiwa katika sare zao na silaha kana kwamba wamesikia habari za magaidi kutaka kulipua eneo la bandari lililopo mkabala na mji huo kumbe ni harakati za kuweka mambo sawa kabla ya kutangazwa yale matokeo yasiyotarajiwa kwa upande wao.

Ushindi huu unafungua ukurasa mpya kwa wachambuzi wa masuala ya siasa za zanzibar kwani mengi yameshaanza kusemwa juu ya ushindi huo wa chama cha CUF kua ni kielelezo cha ushindi mkubwa walioporwa october 30.Ushindi huu wa chama cha CUF unakuja huku kukiwa na matukio kadhaa ya kutisha yaliyotokea jana baada ya wafuasi wawili wa CUF kupigwa risasi sehemu za siri na mwimgine kuchomwa kisu cha tumbo.

Hadi napoandika makala hii mji wa zanzibar katika jimbo la mji mkongwe umezizima kwa furaha huku wananchi wakionyesha tabasamu licha ya kudhibitiwa na vikosi vya kiusalama wanaofanya watu waamini kua ushindi huo wa CUF ni kama dhambi ya mauti kwa chama tawala.

3 comments:

Ndesanjo Macha said...

Nilipomaliza kusoma ripoti yako ya uchaguzi nimetabasamu. Hii moja ya zile "ishara ndogo" kuwa blogu itakuja kuwa na nafasi kubwa sana katika jamii yetu. Huo wakati utafika. Historia ya vyombo vya habari inatuonyesha kuwa vyombo vyote hupitia kipindi cha kukua, kukubaliwa, kupatikana kwa urahisi na kukubaliwa. Kitendo chako, kama raia binafsi, kutupa habari za uchaguzi kama ulivyoziona na sio jinsi "mhariri wako alivyoamua kuwa ni nini ulikiona" au habari kutokana na msukumo baridi wa matajiri wanaowapa matangazo wenye vyombo vya habari, ndio ishara ninayoizungumzia.

boniphace said...

Ndesanjo Materu si mwandishi wa Habari wala hakuwahi kuandikia gazeti lolote. Huyo Mwanazuo wa masuala ya Siasa na sasa akifanya katika kurugenzi nisoijua vema hapo Zanzibar. Huyu ni moja ya mafanikio ninayojivunia. Karibu Materu kaza butu njoo na nyingi mpya

FOSEWERD Initiatives said...

kaka materu,

mungu yupo! demokrasia ina makusudi mazuri kabisa ya kumfanya anayekubalika na kupendwa la kama si mwenye uwezo wa kukomboa watu apewe nafasi! jinsi ilivyo sasa hivi tanzania - bara, ukiwa mpinzani unaonekana kuwa ni mhaini! na mwenye uchu wa madaraka! binafsi ninawapongeza sana wazanzibar kwa kuamua kuchukua mustakabali wa maisha yao mikononi mwao! sielewi kuwa ni nini hasa kinachowafanya watu wapende sana kutawala?? sijui hawakusomea kazi za kufanya? au ni nini!!

walisema ngoma ikipigwa unguja, basi afrika mashariki nzima wataicheza!

lakini ni fundisho kwa wabara, kuwa demokrasia inafanyiwa kazi ambayo hata risasi haitaizuia. kaka materu, tunaendelea kushaurian ni jinsi gani tutawaamsha watanzania kwa kasi mpya ari mpya na nguvu mpya! hakika glubo ni njia ya kwanza.

nimefurahi kutua kwa glubo yako!
cheers!