Saturday, December 31, 2005

KIKWETE ASEMA HALI YA KISIASA ZANZIBAR INAHITAJI MJADALA WA KITAIFA

Rais mteule wa jamhuri ya muungano wa Tanzania bwana Jakaya kikwete jana kwa mara ya kwanza alilihutubia bunge,ikiwa ni siku mbili baada ya kupatikana kwa spika wa bunge hilo na siku moja baada ya uteuzi alioufanya wa ndugu Edward Ngoyai Lowassa kuthibitishwa na bunge kua waziri mkuu wa tisa wa jamuhuri hii ya Tanzania.

Ikiwa kama ni hotuba ya kutoa dira ya serikali yake ya awamu ya nne,mambo mengi aliyazungumzia kwa kina kwa takribani masaa mawili lakini mpasuko wa kisiasa uliopo Zanzibar umeonekana kuchukua uzito mkubwa na kua gumzo katika mitaa mbalimbali ya visiwa hivi ambavyo mchakato wa kisiasa umekua na matatizo makubwa bila kupewa uzito unaostahili.

Kumbukumbu zangu zinanisukuma kusema kua ukiacha mwalimu Nyerere,Jakaya kikwete anakua kiongozi wa kwanza wa ngazi za juu kuzungumzia suala hilo hadharani ambalo linaonyesha kumkera kama si kumkatisha tamaa kwani halitoi muelekeo mwema kwani hali ya chuki inayoendelea kujengeka katika misingi ya Upemba na Uunguja inazidi kuota mizizi kama si kushamiri.

Inawezekana Kikwete amehamasika kupasua jipu hili kufuatia muendelezo wa matokeo ya uchaguzi yanayoendelea kugawa visiwa hivi katikati.Chama tawala(CCM) hakikuambulia hata kiti kimoja katika kisiwa cha pemba ambacho kinaaminika kua ni ngome kuu ya chama cha CUF,huku CCM ikijizolea viti vyote vya Unguja isipokua katika jimbo la mji mkongwe ambalo wapinzani wanaonekan kujizatiti.Nikiwa katika mizunguko yangu ya kawaida katika mitaa ya mji huo mkongwe leo nimeshuhuda makundi mbalimbali ya watu wakijadili hotuba hiyo huku wengi wakijiuliza ikiwa mfupo uliomshinda Mwinyi na Mkapa yeye(kikwete)atauweza???

Naamini kabisa kua haiitaji viongozi wetu kua na shahada za chuo kikuu ili kubaini uzito wa tatizo lililopo visiwani hapa isipokua ushabiki wa kisiasa ndio unawaponza kuchukua hatua za haraka kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili ambalo ni kama bomu linalosubiri mda kulipuka.Cha ajabu ni viongozi hawa kuchukulia mpasuko huo kama silaha ya wao kujijengea umaarufu wa kisiasa na hata kuendelea kuungwa mkono na wanachama wao.

Nimekua nikijiuliza maswali mengi bila ya kupata majibu sawia,Kwanini watu wafike mahali hadi kushindwa kumpangisha mtu nyumba ya kulala kutokana na chuki zilizojengeka katika hali ya upemba na uunguja?Kwanini watu wasusiane maiti kutokana utofauti wa asili zao?Kwanini watu waendelee kupiga kura za chuki bila kuzingatia uwezo wa wagombea wanaowapigia?Kwanini watu waendelee kutofautishana kwa sura na kunyoosheana vidole vya uunguja na upemba?

Fursa aliyoahidi kuitoa Kikwete kujadili mustakabli wa kisiasa katika visiwa hivi, naichukulia kama tunu ya wanablog kuanza kuelekeza fikra zao katika kutoa nafasi ya TAFAKURI makini zinazozingatia suluhisho zaidi ya kuendelea kuhoji matatizo yaliyopo.Nataka tuichukulie nafasi hii kulifanyia jambo taifa letu jambo la neema na matumaini kwa vizazi vijavyo.

21 comments:

boniphace said...

Materu naomba fatilia na utupe kwa kina katika ngome ya CUF wamepokeaje hiyo hotuba na lipi linajadiliwa huko maana najua kulitangazwa kuwa na nguvu ya umma baada ya kuanza hii Januari.

Mija Shija Sayi said...

Unajua hili jambo tunalichukulia kimzaha mzaha, majuzi nilikuwa nazungumza na rafiki yangu mmoja akasema huko Pemba na Unguja hadi ndoa zinavunjika eti kwa sababu tu ulikwenda katika ngome ya CUF au CCM, sikuamini..sasa hii ya kwako ya hadi kususia maiti??..imeniacha mdomo wazi. Haya mambo tusiyachukulie juu juu, mchango wa mawazo unahitajika kwetu sote, tusiwaachie viongozi peke yao.

Ndesanjo Macha said...

Mimi napenda kusubiri kwanza maana hotuba za mwanzoni mwanzoni za Mkapa zilikuwa na ahadi chungu nzima za kubadili mambo. Nakubali kuwa Kikwete katika hotuba yake ametaja mambo ambayo yamekuwa yakizungumzwa kichinichini na watwawala. Ninachofanya ni kusubiri kuona kama ile ilikuwa ni hotuba tu iliyoandikwa na mwandishi wake wa hotuba au ni azma ya dhati ya kutaka kubadili mwelekeo wa taifa letu. Napenda yetu yawe ni macho zaidi ya masikio.

FOSEWERD Initiatives said...

nitaifanyia kazi hotuba hii! nilivyoisikia siku ile kwa furaha nilienda kunywa bia nyingi sana kidogo nikijihisi kuwa ni raia wa nchi na sio muumini wa kanisa! unaweza kuwa ni mwanzo mzuri! ila ninatoa rai wana blogiu tuanze kuichambua hotuma hiyo tukijaribu kufafanua kwa mapana matokea tarajiwa kwa pande zote mbili!

si mnajua kikwete naye anablogu? - tuendelee kumsaidia.

cheers

FOSEWERD Initiatives said...

kikwete ameahidi kuanzisha wizara ya kushughulikia ueaia. kilio chetu cga siku nyingi! alisema mtu asihukumiwe kwa imani ya chama! pia kuondoa sheria mbovu mbovu kumzuia mbowe kama raia yeyote yule asitumie bendera ya taifa!

Jeff Msangi said...

Mark,
Kuna uwezekano wa kuipata hotuba nzima ya Raisi Kikwete iwe kwa sauti au maandishi?Nadhani ni muhimu wanablogu wote tukawa na kopi.

FOSEWERD Initiatives said...

jeff nitaitafuta na nitaipata. pia nitaisambaza. mimi niliisikiliza kupitia

http://www.radiomariatanzania.co.tz

Ndesanjo Macha said...

Muhimu sana kuwa na hotuba nzima. Tuisome, tuichambue, na kuihafadhi maana itakuwa ndio kipimo chetu cha uongozi wake. Yeyote atayeipata atupatie.

Indya Nkya said...

Materu, nimetembelea kibaraza chako safi kaka.

FOSEWERD Initiatives said...

wamenifurahisha sana hawa CUF wameamua kuwatolea uvivu hawa wazembe wengine. kina cheyo out!!!

http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2006/01/03/57109.html

naona kuna muvu kali hapa inataka kuanza. CUF wamewastukia wenzao!!!!unajua bwana kama hawa kina mtikila wenyewe wanauma na kupooza. jana hawa TLP vijana wakamtumia salamu za mwaka mpya karume kuwa alishinda bila mikwaruzo...huoni kuna kitu inaendelea hapo?

FOSEWERD Initiatives said...

fikra uko jikoni tumiminie vitu, tumehama maana ni wewe na miruko sasa

http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2006/01/03/57109.html

Christian Bwaya said...

Hatimaye yule yule mzee (Kikongwe) amerudi tena. Leo si Mshauri wa Rais...hapana. Ni Askari wa Mwamvuli. Mnaonaje hapo jamani?

Fikrathabiti said...

Duh!na kingunge naye ndani!!!!!!!!
Kwasasa ni waziri wa nchi ofis ya Rais anayeshughulikia siasa na uhusiano wa jamii.
Je naye huyu anaweza kwenda kwa kasi mpya tunayoisikia?????

FOSEWERD Initiatives said...

kwa kweli sijui lolote kama alikataa kuwa na dini leo atakubali kukaa meza moja na CUF na Chadema kweli? sijui labda utu uzima dawa!

boniphace said...

Fikra thabiti tumesoma makala hii sasa basi unasubiri nini kurusha kauli za CUF hapo Zanzibar au unasubiri magazeti yakuwahi. Tulishe kaka maana tuna njaa ya taarifa.

Semkae said...

http://www.mbongo.com/Tanzania-commentator/default.aspx

FOSEWERD Initiatives said...

bwana Materu, Picha zenu, Semfue, Makene na wengine kama bado hamujaweka kitu ndani nimewaandalia wahabeshi pale kwangu! karibu muoe!

boniphace said...

Uko wapi Mteru tumechoka kuinghia katika nyumba bila kukuta wenyeji. Hivi lini utaandika tena. Tumechoa tumechoka

FOSEWERD Initiatives said...

Fikra! yaani Unguja na Pemba pamoja na vijimambo vinavyozuka kila siku hakuna stori? kumbuka ni mwanablogu pekee unayewakilisha visiwa! kama hamna za msingi basi tushushie hata za popo bawa!

MICHUZI BLOG said...

yakhe wajifichaga wapi weye, mi naja sana unguja, sijui wapatikanaje atiii...

Fikrathabiti said...

Michuzi mimi nipo sana sheikh unguja na ukinitaka utanipata kupitia 0744-322 245