Thursday, December 22, 2005

ANAYEJIITA MUUMINI WA DEMOKRASIA TANZANIA AANZA KULA MATAPISHI YAKE!
Ukweli na umakini wa utekelezaji ahadi ziltolewazo ni miongoni mwa misingi mikuu ya demokrasia.Ni katika mtazamo huo umenifanya kujenga desturi ya kua na hofu pindi nionapo mtu anaenda kinyume na kile alichoamini,na baya zaidi mtu aliyejijengea heshima na sifa katika jamii husika.

Mwaka 2000,Spika anayemaliza mda wake Mh. MSEKWA alitamka hadharani kua hatagombea tena kiti hicho baada ya kulitumikia bunge kwa takriban muongo mmoja kwasasa na badala yake ataachia wenye mawazo na fikra mpya wachukue hatamu. Sitaki kuamini kua miaka mitano ni mingi sana kiasi cha kumfanya mtu asahau aliyoyasema.

Mh. huyu muumini(Msekwa) ameibuka ghafla na kuweka wazi kua amebadili nia yake ya kustaafu na kutangaza kuchukua fomu kwa ajili ya kutetea kiti hicho.Katika hali ya kustaajabisha ni pale msekwa alivyoonyesha kukerwa na maswali ya mtangazaji wa BBC aliyekua anahoji sababu za yeye kuendelea kung'ang'ania hicho.Mhesimiwa alianza kujibu kwa kuhamaki na kunga'ka kana kwamba mtangazaji yule hakupaswa kumuuliza maswali hayo.

Hii tabia inaonyesha kuanza kuota mizizi baada ya mwaka 1995 Komandoo Salmin Amour,aliyekua rais wa Zanzibar kufika mbali hadi kutaka kubadili katiba ili aendelee kubaki madarakani na bila aibu wiki iliyopita alipokua akihojiwa akasisitiza nia yake aliyokua nayo kipindi kile kwa kisingizio kua wananchi walikua bado wanamuhitaji kama anavyojaribu kutueleza Msekwa kua wabunge walimuomba asing'atuke!

Binafsi naamini kua bunge letu limejaa vipaji vya kila aina vinavyoweza kuijaza nafasi hiyo bila matatizo.Ni jambo la heri kua siku hizi mtu binafsi anaweza kuomba nafasi hiyo jambo linalopanua wigo wa kuibuka kwa vipaji vya raia wa kawaida kuiomba nafasi hiyo.HII NI CHANGAMOTO KWENU mh. NDESANJO NA MAKENE mjitokeze na kuwatoa watanzania kimasomaso kwani nahisi waheshimiwa wa aina ya msekwa ni wale walio na hofu ya kurudi uraiani na kuishi maisha ya kawaida kama tuishiyo sisi.

7 comments:

boniphace said...

Materu unaugonjwa mmoja, mzuri wa kupanga hoja lakini husomi maoni na kuchangia mijadala katika Magazeti Tando ya wenzako. Ingia huku ndugu yangu, ingia sasa ukuze fikra. Kinachonisibu mimi na wewe ni aina ya Elimu ya hapo Mlimani. Haijatuivisha sana na tunatakiwa kulishana fikra kabla ya kuingia kufanya maamuzi makubwa. Huyo mjinga aliye na wivu hata kwa akina Mongella bado anatamani nini?

Mshenzi sana kama nikipata muda hapa nitandika uchambuzi niutume Bongo kupingana na hoja hiyo sasa maana kwa kweli inatia uchungu.

FOSEWERD Initiatives said...

unaona sasa ndiyo yale yale! hawa wazee wakiwa ndani ya system hawataki kutengeneza mazingira mazuri ya watu walio nje ya system. mfano kumbe ili mtu aishi vizuri tanzania ni lazima awe msistimu! kama wao wako ndani ya systimu wanajipangia mishahara mizuri, wanajipa magari manene, wanajipa maalawansi mazito mazito, wanaacha kupigania maisha bora kwa kila mtanzania! ona wamewasahau madaktari leo hii wananyanyaswa, ona wanasahau vijana wanaomaliza masomo, ona wanasahau kumpigania mkulima bei nzuri, ona wanawaacha wasanii wanaibiwa, ona wanakazana kulipa madeni wanaacha wanachi hawana hata senti nyekundi mfukoni, ona wanaacha hospitali zinakufa, ona wanaacha watu hawana ambulance!! ONA WANAKAZANA KUZIBA FIKRA ZA WATU HUKU WANADAI UTANDAWAZI UNAINGIA!!!mheshimiwa msekwwa yeye akiwa kiongozi wa watunga sheria na wapitisha bajeti, aliliacha hilo akiwa kwenye nafasi stahili ya uspika anaanza kuhangaika sasa atafanyaje kwa sababu bila hivyo maisha yatamgonga tu!!VX ile lita moja kilomita 4 ataweza wapi?? hapo bado hujafungulia AC! mheshimiwa msekwa anawakilisha sehemu kubwa ya viongozi waliolamba madume kupitia CCM. wengi wameenda pale kupooza njaa zao, na wenyewe huwaga wanajihakikishia wakishapita kwenye mchujo wa chama tu wamelamba dume! na watanzania wao wanachagua chama cha nyerere!!! nani kama chama? shauri yenu hamjui kimeingiliwa siku hizi!watanzania sasa tuamke, kwa kuanza sikiliza agenda ya kwanza ya bunge tukufu ni kupandisha mishahara. sawa niliHISI kikwete angeshinda lakini nilisikitika ile kampeni ya mafiga matatu - chagua raisi, mbunge na diwani kwani imewabeba wabinafsi kibao! yangu macho.

Fikrathabiti said...

Kaka makene nashukuru sana kwa kuniunga mkono katika jitihada zangu za kufufuka kutoka katika dimbwi la fikra chakavu zisizo na matumaini mema kwa taifa letu.

Nakufahamu wewe si kama ndugu tu bali pia kama mmoja wa mwanaharakati halisi uliye na uchungu na Tanganyika yetu iliyoasisiwa na wazee wetu nyakati za ASP na TANU.

Ila punguza ukali wa maneno kwa kutumia TASHBIHA jengevu inayokemea maovu yote katika ardhi yetu.Hapa namaanisha kua neno"MSHENZI"sikulipenda.

Nakaribisha ufafanuzi juu ya matumizi ya neno hilo.

Ndesanjo Macha said...

Sikujua kuwa Mswekwa alishatamka kuwa hatakamata tena kiti cha uspika, yaani ufalme wa bunge, wa bunge Tanzania. Amefanya kiti hicho mali yake sio? Hii habari ya nguvu mpya blah blah ni kuuziana maneno tu.

Ndesanjo Macha said...

Umesema utafanya juu chini kukutana na mwanablogu mwenzio Kaka Pori uendapo Dar. Jambo zuri sana hili kukutana ana kwa ana na kupanga mikakati zaidi. Mtakapokutana mtupe mrudisho nyuma wa kikao chenu.

Najua Jeff na Boniphace watakutana karibuni. Najua watapanga mengi mazuri.

FOSEWERD Initiatives said...

kaka ndesanjo, mrudisho nyuma si ndio hadidu za rejea? kipi sasa ni sahihi zaidi?

Fikrathabiti said...

Kwa kweli kaka Mark na Ndesanjo sina budi kusema kua mnazitajirisha fikra zangu na misamiati ya kiswahili.
KISWAHILI JUUU,JUUU ZAIDI
Kidumu kiswahili na si vyama TAWALA!!!!!!!