Tuesday, December 27, 2005

VITA YA KIFIKRA

Ulingoni naingia,hoja kutoani
Africa yangamia,tuingie vitani
Viongozi hatarini,bongo zao usingizini
Hima hima jikazeni,mda hausubirini!

Fikra chakavu nazungumzia,zilizochoka chambua
Uzandiki ndo umezijaa,zisizojali raia
Kila siku kutuhadaa,na hadith zisizoisha
Hima hima jikazeni,mda hausubirini!

Makene twasubiria,mstari wa mbele jitokeze
Ndesanjo nawe fatia,ili wengine wajitokeze
Hali sasa yachefua,ujinga tutokomeze
Hima hima jikazeni,mda hausubirini!

Tusikate tamaa,daima mbele tusonge
Vizazi kuokoa,fikra zao tuzijenge
Rai nazidi toa,wanablog wajiunge
Hima hima jikazeni,mda hausubirini!

Fikra chambuzi ndo silaha,mimi nasisitiza
Hakuna msamaha,tutaotoa kwa bongolala
Wote tuangamize,vionngozi ndo nazungumzia
Hima hima jikazeni,mda hausubirini!

ALUTA CONTINUE!!!!!!!!!!
NB:Mwalimu makene nakaribisha masahihisho na maoni katika masuala ya vina na mizani.

6 comments:

boniphace said...

Karibu mshairi Materu, kweli fani imeingiliwa sasa? Fikra thabiti zinachanja mbuga kiushairi. Sitachanganua lolote kuhusu vina na mizani sasa maana kuna mashairi guni au mapingiti kama anavyoyaita Andanenga na wenzake. Ushairi si fani tu bali maudhui na katika hili nakupa heko.

Siku hizi wito wangu na huu ni wito wa mwaka mpya kwa kila mmoja wetu kwamba tuhamasishe umma wa watanzania kurejesha utamaduni wa kujisomea vitabu. Ugonjwa wea kutosoma ndio huu unaofanya fikra chakavu kuhenziwa kwa miaka na miaka. Amka wewe waweza nunua kitabu kimoja kila baada ya miezi mitatu na kukisoma na kisha kuwatafuta wengine nao kusoma wakati ukiendelea kublog.

Amka sasa mapambazuko hayakungoji.

FOSEWERD Initiatives said...

mpendwa materu,

sawa hasa, haya mawazo chakavu ndio yale ambayo muheshimiwa Freeman Mbowe anayaita mawazo mgando! - lazima tuwe tindikali za kuyayayusha mawazo ya namna hii!!

FOSEWERD Initiatives said...

hivi nilisahau kukuuliza. wewe mwenzetu ambaye uko unguja unajisikia sikiaje kuona hao jamaa walivyokataliwa kiongozi wampendae?

Fikrathabiti said...

Brother mark,hao kwa upande wao ni kilio na kusaga meno huku waliong'ang'ania hatamu ni sherehe na kejeli zisizoisha zinazonakshiwa na TAARAB kila kukicha mitaani

Kwasasa hawa wenzetu wa CUF walipokutana wiki iliyopita walitoa tamko kali la kutotambua matokeo ya Zanzibar na Muungano na kutangaza rasmi kuuzika muufaka wao na chama tawala.

Wametangaza pia wataitisha nguvu ya umma nchi nzima hapo january kama njia ya kudhihirishia dunia kua kile wanachodai kina mantiki.

Tusibiri tuone ila kama nijuavyo ni vipigo tu vitatawala na yale yaliyojiri Jauary 26 na 27 yamaweza kujirudia kwa ARI MPYA,NGUVU MPYA NA KASI MPYA.

FOSEWERD Initiatives said...

Aksante sana kaka materu kwa ufahamisho huo. unajua kaka hata kama mimi nipo mwanachama wa chama tawala lakini ninaona hiki wanachofanya kina mang'ula ni kitu cha hatari sana sana kwetu sisi na watoto wetu. kitendo cha mimi kuunga mkono udhalimu ni usaliti mkubwa kwa watanzania na watoto wetu. wanataka kufika mahali hata raisi mpya akitoka upinzani iwe ni kama mapinduzi ambapo serekali yoote na watu woote wanaoitumikia sasa hivi watatupwa nje wakati hata wazuri wapo. nilimsifu shariff alikuwa na nia nzuri tu ya kuunda serekali ya mseto. maana yake alikubali kuwa mema ya CUF na CCM yaonekane kwa umoja kwa wananchi. watu ni wale wale tofauti ni vyama tu! tunataka mabadiliko ambayo ni smooth kiasi kwamba mabadiliko ya oungozi katika nchi yasiandamane na visasi. kwa mfano, jichukulie wewe umeupata uraisi hata kwa tiketi ya CUF. je una imani na polisi wakiojiunga na kundi la janjaweed?

umesema wataitisha nchi nzima hata bara? - nadhani hiyo ni muhimu sana. na hao waangalizi wa kimataifa waje watoe maoni bila kusahau BBC na CNN! - hatutaki upumbavu sasa! hata magazeti yetu ya ndani ya nchi yametusaliti! sijui hawa wenzetu hawana uwezo wa kuzaa au si wazazi?? mbona hawawafikirii watoto zao?

FOSEWERD Initiatives said...

fikra Dhabiti

je unaweza kunipa kalink nifuatilie hii habari ya maazimio ya cuf?